Wasifu wa marehemu DKT John Pombe Magufuli

 


 

John Pombe Joseph Magufuli alikuwa rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Alichaguliwa Oktoba 2015 na kurithi mikoba ya Jakaya Mrisho Kikwete. Alikuwa mwanasiasa mwenye sifa ya uchapakazi na asiye na mazaha.

Matangazo ya kibiashara

Magufuli au JPM kama alivyofahamika, alichaguliwa kwa mara ya kwanza 1995 katika nafasi ya ubunge, na akahudumu katika baraza la mawaziri katika nafasi ya naibu waziri wa ujenzi kuanzia 1995 hadi 2000, waziri wa ujenzi kuanzia 2000 hadi 2006, waziri wa ardhi na maendeleo ya makaazi mwaka 2006 hadi 2008, na waziri wa ujenzi kwa mara ya pili kuanzia 2010 hadi 2015. Akisimama kama mgombea wa chama tawala - Chama cha Mapinduzi CCM, alishinda uchaguzi wa mwaka 2015 kwa kura 8,882,935 na aliapishwa Novemba 5, 2015 kuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akilihutubia taifa usiku wa Februari 17, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alisema Magufuli alifariki majira ya saa 12:00 jioni kutokana na tatizo la moyo.

Amesema kwamba rais Magufuli aliaga dunia katika hospitali ya Mzena iliyopo jijini Dar es Salam mwendo wa saa kumi na mbili jioni saa za Afrika Mashariki kutokana na matatizo ya moyo.

Kwa mujibu wa makamu huyo wa rais Magufuli alikuwa chini ya uangalizi wa madaktari wa moyo kutoka hospitali ya Jakaya Kikwete.

 

No comments:

Post a Comment