Lissu Atangaza Nia ya Kuwania Urais 2020





Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu leo amezungumza kwa Mubashara kupitia ukurasa wake wa Facebook akiwa ughaibuni na kutangaza nia ya kugombea Urais nchini Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa October 2020.

Lissu amechukua hatua hiyo siku kadhaa tangu John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema, kuwataka wanachama wenye nia ya kugombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho, kuwasilisha taarifa zao katika ofisi yake, kuanzia tarehe 3 hadi 15 Juni 2020.

Lissu amesema, endapo atafanikiwa kuwa Rais, ataboresha uchumi wa nchi, mahusiano na jumuiya za kimataifa na nchi marafiki, utawala bora, misingi ya haki za binadamu, demokrasia na mfumo wa vyama vingi.

Amesema uchaguzi wa mwaka huu, utaamua kama Chama cha Mapinduzi (CCM), kitapata fursa ya miaka mitano mingine ya kuendelea kuharibu uchumi wa nchi na kufukarisha wananchi, au mwanzo mpya kwa Tanzania, kujiimarisha kiuchumi.

Lissu amesema, akifanikiwa kuwa Rais wa Tanzania, atahakikisha mihimili ya nchi, ikiwemo Bunge na Mahakama, inakuwa huru na kujitegemea kwenye maamuzi yake.

Amesema katika uongozi wake kama atafanikiwa kuwa Rais wa Tanzania, atavitumia vyombo vya ulinzi na usalama kulinda haki za binadamu, na si katika kukandamiza wapinzani wake, vyombo vya habari na asasi za kiraia.

Amesisitiza kuwa endapo atafanikiwa kuwa Rais, Serikali yake itaendeshwa kwa kufuata misingi ya utawala bora na sheria, inayoendana na Katiba ya nchi pamoja na mikataba ya kimataifa, ambayo Tanzania iliikubali.

Lissu amesema, akifanikiwa kuwa Rais wa Tanzania, ataponya majeraha ya wananchi pamoja na kurejesha umoja wa kitaifa, huku akisisitiza kwamba hatalipa kisasi kwa maadui zake.


(GLOBAL PUBLISHER JUNE 8 2020)
Read More

Waziri Ummy Mwalimu: Serikali imefanikiwa kudhibiti corona








Serikali imesema kuwa imefanikiwa kudhibiti na kupunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi ya virusi vya corona huku ikiwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ili kuutokomeza kabisa.

Hayo yalisemwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa ziara yake ya kushtukiza kwenye kwenye Kituo cha Afya cha Ngamiani Jijini Tanga ambapo aliweza kuzungumza pia na wahudumu wa Afya na kupokea msaada wa vifaa vya kunawia maji kudhibiti Ugonjwa wa Covid 19 vilivyotolewa na Shirika la Water Mission Tanzania.

(MUUNGWANA BLOG, june 2020)
Read More

Rais Magufuli atajwa kati ya watu 10 walioleta mabadiliko Afrika






Utendaji kazi wa Rais John Pombe Magufuli unaendelea kuonekana nje ya mipaka , baada ya Jarida kubwa la African Report kumtaja Kama miongoni mwa watu 10 walioleta mabadiliko makubwa barani Afrika

Jarida hilo limemtaja Rais Magufuli kama kiongozi aliyeweza kufanya mapinduzi makubwa katika miradi ya Kiuchumi na kijamii , na kusababisha uchumi wa Tanzania kua ni uchumi unaokua kwa kasi zaidi barani Afrika

Pia limemuelezea Rais Magufuli Kama kiongozi aliyeweza kurejesha nidhamu ya kazi kwa viongozi wa umma, kudhibiti rushwa na Kupunguza matumizi mabaya ya kodi za wananchi

Vilevile limesifia juhudi zake za kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji nchini Tanzania, pamoja na kujitolea kupunguza mshahara wake kipindi alipoingia madarakani.


MUUNGWANA BLOG, JUNE 7 2020
Read More

Ujerumani yasubiri taarifa rasmi ya Marekani






Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Annegret Kramp-Karrenbauer amesema Ujerumani haijapokea taarifa rasmi kutoka Marekani kuhusu mpango wa nchi hiyo kuwaondoa baadhi ya wanajeshi wake Ujerumani.

Akizungumza leo na waandishi habari, Kramp-Karrenbauer amesema hawezi kuzungumzia taarifa za kwenye vyombo vya habari bila ya kuwepo uthibitisho.

Kiongozi huyo wa chama cha Christian Democratic Union, CDU amesema ukweli ni kwamba uwepo wa majeshi ya Marekani nchini Ujerumani unatumika kuimarisha usalama wa Jumuia ya Kujihami ya NATO na washirika wengine wa NATO pamoja na Marekani yenyewe.

Amesema huo ndiyo msingi ambao unaleta ushirikiano wa pamoja kati ya nchi hizo. Naye msemaji wa serikali ya Ujerumani, Steffen Seibert amesema Ujerumani itatoa tamko mara itakapopewa taarifa na Marekani.

Siku ya Ijumaa, afisa wa ngazi ya juu wa Marekani, alisema kuwa Rais Donald Trump aliliamuru jeshi la Marekani kuwaondoa askari wake 9,500 kutoka Ujerumani.

(MUUNGWANA BLOG, June 2020)
Read More

Corona imeisha tutafungua Shule za Msingi na chekechea hivi karibu- JPM





“Tulitaka kumpa utawala shetani badala ya kumpa Mungu, nawashukuru Watanzania kwenye corona tumeshinda, nina uhakika hivi karibuni baada ya kufungua vyuo tunaangalia mambo yanavyoenda na shule za msingi, chekechea na nini,  nazo ziko mbioni tutazifungua”-JPM

“Tuko pamoja na Walimu, shida tunazijua, nikisahau Mwl. Majaliwa ananikumbusha, akisahau Mhagama anamkumbusha, akisahau anakumbushwa na Mwl Ndalichako au Mwl Mkuchika wakisahau wote hata Mkewe Mama Majaliwa anamkumbusha Majaliwa mahali pema pa kukumbushwa”-JPM

(MUUNGWANA BLOG, June 5 2020)
Read More