
Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na
kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi
kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa
pamoja kwa kipindi chote cha maisha.
Wanawake wengi wanajisahau
na kudhani kwamba kitu kinachoweza kuwafanya wakapata wachumba ni uzuri
hivyo kupoteza muda wao kujichubua na kujiremba ili wawavutie wanaume
bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri.
Hali sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma
ambapo ukiwa na sura nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za
kuolewa.
Utafiti ambao nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzuri
wa tabia na umbo, kuna kuna sifa nyingine za msingi ambazo mwanamke
anatakiwa kuwa nazo ili aweze kuwa katika mazingira mazuri ya kupata
mchumba wa kumuoa kiasi kwamba asipokuwa nazo ataishia kuchezewa tu
lakini haitatokea mtu kumtakiwa kwamba anataka kumuoa.
1. Mwenye mapenzi ya kweli.
Lengo
kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa
mwanamke na ikiwezekana waweze kupata watotoa ambapo watoto hao ndio
furaha ya ndoa. Wapo wanawake wengine ambao wanonesha wazi kutokuwa na
mapenzi ya kweli bali wanakuwa na mapenzi ya kuzuga. Wanachotaka wao
aidha kupata umaarufu tu kwamba yuko na mtu fulani ama kuweza kupata
pesa alizonazo mwanaume lakini sio kwamba ana mapenzi ya dhati kutoka
moyoni mwake.
Mwanamke asiye na mapenzi ya dhati utamgundua tu,
muda mwingiutamuona macho yake yako kwenye mfuko wa mwanaume. Akiona
kwamba mfuko umetuna utaona anaonesha mapenzi ya hali ya juu lakini
pindi hali inapokuwa kubwa mbaya kifedha mapenzi yanaanza kufifia.
Kwanini
wanaume wanapenda wana wake wenye mapenzi ya dhati kutoka mioyoni mwao
na si kutokana na fedha walizonazo? Hii inatokana na ukweli kwamba
maisha siku zote yanabadilika, kama waswahili wanavyosema, kuna kupanda
na kushuka.
Sio kwamba kila siku utakuwa na maisha mazuri na kama
itatokea hivyo basi ushukuru mungu.Hivyo basi mwanamke wa kuoa lazima
afahamu hivyo na awe tayari kuonesha mapenzi yake ya dhati wakati wote
wa maisha yao na si kwa kipindi fulani tu cha neema.
Si hivyo tu
pia asilimia kubwa ya maisha ya ndoa yanatawaliwa na mapenzi, kwa hiyo
nyanja hiyo inakuwa ya msingi sana kwa wanaume wengi kuiangalia ili
wasije wakajikuta wanaoa mwanamke ambaye baada ya muda mapenzi
yanakwenda likizo hali ambayo inaweza kuwafanya wasiishi maisha ya raha
mustarehe.
2. Wenye tabia nzuri
Tabia njema ndio
silaha ya maisha, ukiwa na tabia nzuri kila mtu atakupenda, hiyo ni
katika maisha ya kawaida. Lakini linapokuja sualana kuoa tabia inakuwa
kitu cha awali sana kungaliwa na hiyo inaweza kuwa na ukweli kwa sababu
wapo wasichana wazuri wenye mvuto wa aina yake na maumbile mazuri,
lakini wanakosa wanaume wa kuwaoa, ukiuliza kwani utaambiwa anatabia
mbaya.
Naweza kusema hilo ndilo limekuwa tatizo kubwa kwa baadhi
ya wanawake kukosa wanaume wa kuwaona. Hakuna mwanaume hata mmoja kati
ya wale ambao nimejaribu kuongea naye ambaye ameonesha kulidharau suala
hilo la tabia.
Si hivyo tu wapo wanaume ambao wameingia kichwa
kichwa na kuoa kwa kuangalia sura tu bila kujali tabia, matokeo yake
baada ya siku chache yanatokea machafuko ya aina yake hali ambayo
imepelekea kuvunjika kwa ndoa kutokana na tabia mbaya alizonazo
mwanamke.
3. Mwenye uchu wa maendeleo
Hivi karibuni
kumekuwepo na mabadiliko ya aina yake kwa wanaume, wengi sasa hivi
hawapendi kabisa kuoa mwanamke ambaye hana kazi yaani ‘golikipa’. Kama
atakuwa hana kazi basi awe na uchu wa maendeleo kwa kujituma kufanya
kazi mbalimbali za kimaendeleo kama vile kilimo kwa wale walio vijijini
na biashara ndogondogo kwa wale ambao wako mijijini na hata vijijini.
Ile
dhana ya kusema mwanamke ni mama wa nyumbani wa kukaa na kujipodoa
akimsubiria mwnaume arudi amstarehesha, sasa hivi imepitwa na wakati.
Wanaume wengi wanapenda wanawake ambao ni wahangaikaji, wenye ndoto za
maendeleo katika maisha yao. Hata kama watakuwa si wafanyakazi lakini
wawe wenye kutoa ushauri kwa waume zao juu ya jinsi gani wafanye ili
wafanikiwe.
4. Wasiopenda makuu.
Kuna wanawake
wengine wanakuwa na tabia za ajabu sana kiasi kwamba yaweza kuwa kero
kwa wanaume. Wapo wanawake ambao wanapenda makuu bila kujali hali halisi
ilivyo. Kuna wanawake naweza kusema wana tamaa, kila wikiendi utamsikia
“leo tunakwenda wapi dear?”
Akimuona rafiki yake kanunua simuya
laki tatu na yeye utamsikia akisema, ‘na mimi naomba uninunulie simu
kama ya Grace’. Ukienda naye Pub anakuambia,”mimi sinywi pombe za chupa
natumia za kopo tena Heineken’. Yeye hajali kiasi cha pesa mwanaume
alicho nacho na usipotekelezea anachukia na anaweza hata kupunguza
mapenzi.
Wanawake kama hawa wako katika mazingira magumu sana ya
kuweza kupata wanaume wa kuwaoa. Mara nyingi katika maisha fedha
huzungumza, kama mwanaume atakuwa na pesa ya kutosha itakuwa rahisi sana
kwa mwanamke kupata kila atakachopenda lakini si kwa kumwambia mimi
nataka kitu fulani.Mwanaune mwenyewe utamsikia akisema, ‘unataka
nikununulie simu ya aina gani, au leo unataka twende wapi?’ hapo ndipo
utakuwa na nafasi ya kusema, ‘mimi nataka uninunulie simu kama ya fulani
ama leo nataka twende sehemu fulani.’
Wanaume ni warahisi sana wa
kuwapatia wale ambao wanatarajia kuwaoa chochote ambacho watahitaji
kama tu pesa haitakuwa tatizo. Kitu ambacho kinawaudhi wanaume wengi ni
ile tabia ya mwanamke kupenda mambo makubwa bila kuangalia uwezo uliopo
kwa mwanume.
Kuna wanawake wengine wao si wasemaji kabisa, yeye
anasubiri leoamemletea hiki, anapokea na kushukuru, kesho akiambiwa
twende beach anakubali. Au wengine wanasubiri mpaka waulizwe wanataka
nini, ndio wanasema.
Sisemi kwamba uwe mkimya tu hata kama una
shida ya kitu fulani na unafahamu kwamba ukimweleza mwenza wako anaweza
kukusaidia, hapana! kama unaona kwamba uwezekano wa kupata kile ambacho
unakihitajiupo mweleze kwa utaratibu naamini atakuelewa na
kukutimizia.Tabia ambayo hawaipendi wanaume wengi ni ile ya kulazimisha
ufanyiwe kitu fulaniwakati inawezekana uwezekano haupo.
5. Wavumilivu.
Wapo
wanawake ambao sio wavumilivu kabisa katika maisha.Tunajua kwamba
maisha siku zote hayatabiriki, yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama
kifedha.Huu ndio wakati wa kuona uvumilivu wa mtu.Kama mwanamke
anatarajia kwamba siku zote ni za raha tu na pindi matatizo yanapotokea
anachukua uamuzi wa kumtoroka mwanume, huyo siyo mwanamke wa kuoa.
Wangapi
leo hii huwatoroka waume zao pindi inapotokea kuumwa, kufilisika ama
kupatwa na tatizo lolote ambalo kwa namna moja ama nyingine yanaweza
kuwafanya maisha yao kutingishika?
Uvumilivu kwa mwanamke
utakuwepo kama tu atakuwa na mapenzi ya dhati kama nilivyozungumza hapo
awali. Mwanamke mweye mapenzi ya dhati ni lazima atakuwa mvumilivu na
atakuwa tayari kuishi katika maisha ya aina yoyote, yawe ya raha ama ya
starehe.Hawa ndio wale ambao wanaume wengi wengependa kuwa nao maishani
mwao.
Kwa maana hiyo basi hiyo iwe changamoto kwa wanawake. Wajue
kwamba wanaume wanafurahi kuwa na wanawake wa aina gani. Hata kama
utakuwa umeshaolewa, kama kuna wakati kunakuwa na kutokuelewana baina
yenu, chunguza yawezekana kwamba unakosa mojawapo ya tabia ambazo
nimezitaja hapo juu. Waweza kubadilika kwani inawezekana.
SOURCE MUUNGWANA BLOG