Katika makala hii hii utajifunza vyakula mbalimbali ambavyo wanaume
hawatakiwi kula ili kubaki na afya bora wakati wote. Kuna vingine
unaweza kuwa unavitumia kila siku bila mwenyewe kujuwa.
Punguza kula vyakula feki kuzuia kupoteza nywele
Moja ya matatizo makubwa upande wa urembo kwa wanaume ni kupoteza
nywele (upala). Lakini kama unatafuta kitu cha kukilaumu dhidi ya tatizo
lako la kunyonyoka nywele basi ni hiyo sahani yako ya chipsi unayokula
kila siku. Vyakula feki (junk foods) ni hivyo vinapatikana kwenye fast
foods na takeaway centers nyingi hasa mijini kadharika vyakula vile
vyote vya kwenye maboksi.
Vyakula hivi feki vina kiasi kingi mno
cha lehemu (cholesterol) na lehemu hii hupelekea kile huitwa kwa
kitaalamu kama ‘pregnenolone’ na kupelekea kiasi kikubwa cha
‘dihydrotestosterone’ (DHT) na hatimaye kupotea kwa nywele kichwani
a.k.a upara.
Kunyonyoka kwa nywele kunaweza kuwa ni jambo la kurithi
(genetics) lakini vile vile aina ya chakula unachokula kinaweza kuwa
kinahusika moja kwa moja.
Punguza kunywa pombe
Wanaume
wengi wanaokunywa bia kupita kiasi huwa na uwezekano mkubwa wa kupatwa
na tatizo la kuota matiti kama wamama tatizo lijulikanalo kwa kitaalamu
kama ‘gynecomastia’.
Kwenye bia au pombe mara nyingi hakuna lishe
ya moja kwa moja na hivyo hukufanya ujisikie njaa au hata kuongzeka kwa
njaa zaidi na ndiyo sababu unaambiwa kama huna uhakika utakula wapi ni
bora usinywe pombe ili kulinda afya yako.
Kwenye bia kuna kitu
kama homoni ya oestrogen ya kupandikizwa na hivyo unywaji pombe kupita
kiasi kuna uhusiano wa moja kwa moja na matokeo ya wanaume kuwa na
matiti kama wanawake.
Acha kutumia mafuta ya mboga mboga kuepuka saratani ya tezi dume
Mafuta
yatokanayo na mboga mboga au mimea yamekuwa yakipigiwa debe kwa miaka
mingi na watu wanaojihusisha na lishe na wale wenye hasira sana na
mafuta yatokanayo na wanyama. Hata hivyo leo nakujulisha mafuta hayo si
salama sana kutumika na mwanaume kila siku. Hili limekuja hasa kutokana
na kuongezeka kwa magonjwa ya moyo na lehemu na watu walazishwawa
kutumia mafuta ya namna hiyo.
Lakini mafuta haya ya mboga mboga
ndiyo kitu kibovu kabisa unatakiwa kukiepuka ili usipatwe na saratani ya
tezi dume. Linapokuja suala la kujilinda saratani ya tezi dume basi
mafuta yenye omega 3 ndiyo suluhisho la kudumu na siyo omega 6 kama
ilivyo kwenye vyakula vingi vya kwenye makopo, mafuta ya alizeti,
maharage ya soya, mafuta ya canola na mafuta ya corn na mengine yote
yenye omega 6.
Popcorn
Popcorn au bisi ni chakula
kingine mwanaume hatakiwi kula, hupikwa kwa kutumia mafuta yasiyo na
afya, sodiamu nyingi na ni chanzo cha baadhi ya kansa. Kuna kitu
kinaitwa ‘Diacetyl’ kinachopatikana kwenye popcorn ambacho kinahusika na
kusababisha kansa na kuna kingine kiitwacho ‘Perfluorochemicals’
ambacho huathiri tezi ya thyroid na ugonjwa wakati huo huo husababisha
ugonjwa wa kupungukiwa umakini ujulikanao kwa kiingereza kama
‘Attention-deficit/hyperactivity disorder (ADHD)‘.Ni vizuri kuacha kula
popcorn.
Mkate mweupe
Mkate mweupe una wanga mwingi
zaidi usio na faida. Kwenye hatua za kutengeneza mkate mweupe vitamini
zote za kundi B hupotea, hupotea pia nyuzinyuzi (fiber). Siyo hivyo tu
mkate mweupe umesemekana kuwa ni sababu ya ugonjwa wa kisukari na
kuongeza uzito zaidi mwilini wakati huo huo ukisababisha tatizo la
kufunga choo au kupata choo kigumu sana.
Vingine vinavyofanana na
na hilo ni ugali wa sembe, tambi nyeupe, chai ya rangi na kahawa. Kula
mkate ambao ngano yake haikukobolewa (brown bread), kula ugali wa dona
na chai unaweza kutumia tangawizi au mdalasini badala ya majani ya chai.
Chumvi ya mezani
Chumvi
ya mezani ile ya unga nyeupe haifai kwa mwanaume. Kila mmoja amesikia
chumvi hii husababisha shinikizo la juu la damu na pamoja na hayo bado
sehemu kubwa ya watu wanatumia chumvi hii.
Chumvi ya mezani
husafishwa kwa kuondoa madini, madini na hupitishwa katika joto la nyuzi
joto. Kwa hiyo uliyonayo sasa ni asilimia 40 ya sodiamu na asilimia 60
ya kloridi, na kisha kemikali kama vile ‘aluminium silicate’ huongezwa
ili kuifanya isishikane na hivyo kubaki katika hali ya unga. Aluminium
silicate ni sumu kali inayoharibu mfumo wetu wa fahamu. Inatajwa kuwa ni
miongoni mwa sababu zinazosababisha ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu
(Alzheimer).
Chumvi ya mawe ya baharini ile ambayo haijapita kiwandani (unrefined sea salt) ndiyo nzuri zaidi kwa afya ya mwanaume.
SOURCE, MUUNGWANA BLOG, 27/3/2021
No comments:
Post a Comment