ANGALIZO


WEBSITE HII IPO KWA AJIRI YA WAKRISTO WOTE. HAIFUNGAMANI NA DINI AU KANISA LOLOTE LILE.

Contact Us

Christian Online Services Organization
P.O.Box 212
Bagamoyo - Pwani
Tanzania

Email: christianonlinetz@gmail.com



POWERED BY:
TCDI

Contact Us

Name

Email *

Message *

Web Traffic


CONTACT US TO BE LISTED ON CHIRISTIAN MAGAZINE

CONTACT US TO BE LISTED ON  CHIRISTIAN MAGAZINE

Search

Blog Archive

Christian Online Membership

Follow us on Facebook

Kwanini ndoa nyingi leo zimejaa migogoro?

 



Mchungaji Peter Mitimingi akiwa na mkewe Patience

Ndoa katika jamii za kikristo zilikusudiwa kudumu na kuwa mfano wa kuigwa na ndoa za watu wengine katika jamii. Lakini cha kushangaza ndoa nyingi leo za kikristo zinavunjika kwa kasi ya kushtusha. Hii inashtusha na kushangaza kwa sababu sisi kama wakristo tumeacha kutembea katika mpango kamili wa Mungu. Kwanini hali hii inatokea? Kuna sababu nyingi kwanini ndoa zinakuwa na migogoro isiyoisha na ningine kutawanyika. Kuna sababu ndogo ndogo na zingine ni kubwa na za msingi.

Zifuatazo ni baadhi ya Sababu Kwanini Ndoa nyingi siku za leo zimejaa Migogoro, Marumbano na Kuvunjika vunjika.

USIOE AU KUOLEWA KWASABABU YA KUMSAIDIA MTU FULANI AU KUMUONEA HURUMA

1. Kuoa au Kuolewa na Mtu kwasababu ya Kumuonea Huruma.

• Kuoa au kuolewa na mtu kwa sababu ya kumuonea huruma ni moja kati ya sababu zisizo sahihi. Na inaonekana kuwa ni sababu moja ya kijinga pia.

•Ndoa zianazo oana kwa misingi ya kumsaidia mtu au kumwonea mtu huruma huwa hazina maisha.

2. Huruma ya Kujiona kuwa ni wewe Ndio Unawajibika.

Kumhurumia mtu na kujiona kuwa una wajibu wa kumsaidia ni vizuri, lakini kuolewa naye kwa sababu hiyo ni wazi kuwa ni jambo lisilo la hekima kabisa.


3. Ndoa niyathamani Kuliko Huruma ya Mahusiano.

• Ndoa ni kitu cha thamani zaidi kuliko mahusiano ambayo yamejijenga katika huruma.

Chukulia kwamba kama mhusika ana masaa sita tu kuishi baada ya ndoa. Kwa hiyo utaishi katika ujinga huo kwa masaa sita tu maana kinyume na hapo utaishi maisha yako yote ukiwa unajihisi mjinga zaidi na mwenye huzuni.

• Hiyo itakuwa ni sabau ya kuvunjika kwa ndoa hiyo kwa sababu utaonekana mbaya zaidi ya kabla hujaingia.


4. Kuoa au Kuolewa kwajili ya Kumsaidia Mtu Anayeteseka.

•Usioe au kuolewa na mtu eti kwasababu unaamua kumsaidia kutokana na shida Fulani.

• Mfano kuna baadhi ya watu utakuta mwanaume anaamua kumuoa msichana fulani eti kwasababu kule anakoishi wanamnyanyasa na kumtesa so anaamua amsaidie amuoe ili aishi naye.

• Hii ni sawa na ile ya ujinga wa kufikiri kwamba utaoa au kuolewa na mtu kwa matumaini kwamba utambadilisha mtu baada ya kuolewa au kumuoa ili afanane na wewe, dini yako au tamaduni zako.

• Kumbuka kwamba, kuwa na jitihada za kukubaliana sio kubadilika, sababu suala ndoa halina haja ya kuweka mabadiliko kwa mtu yeyote.

• Ukitaka kumbadilisha mwenzi wako usisubiri kwenda kumbadilishia ndani fanya hayo mabadiliko kabla ya kuingia ndani.


–Mchungaji Peter Mitimingi

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © Christian Online Services - East Africa. Designed by OddThemes