Kumuamsha mdada wa kazi saa 11 alfajiri na kuwaacha binti zako wamelala Ni kumuandaa binti wa kazi kuwa mke Bora kuliko wanao.
Eti kumtumikisha dada wa kazi apige deki, apike, afue nguo, aoshe vyombo wakati wanao wanaangalia TV. Ni kumuandaa mdada wa kazi kuwa mwanamke anayewajibika kuliko wanao.
Kumuacha binti wa kazi aandae watoto kwenda shule, awaandalie uji mapema, awalishe, awasafishe wakati wanao wanacheza gemu kwenye simu au computer Ni kumuandaa binti wa kazi kuwa mama na mlezi bora kwa watoto kuliko wanao.
Na kwakuwa yote hayo unayafanya kwa masimango na manyanyaso unamfanya mdada wa kazi kuwa jasiri mwenye kuzikabiri changamoto za ndoa yake kuliko wanao.
Ukimaliza kwa kusema mwanao akiwa hajui hayo yote, ndoa ikiharibika mnazunguka kutafuta maombi kwa wachungaji kumbe ninyi mmeharibu ndoa za watoto wenu.
Msiwasumbue wachungaji bali wewe kama mzazi mfundishe mwanao kufanya kazi kama vile afanyavyo mdada wa kazi ili naye mwanae aje kuwa mke mwema hapo baadae.
No comments:
Post a Comment