Tangawizi
ni mmea kati ya mimea mingi yenye maajabu, Mmea huu unaweza kutumika
kama dawa na kutibu magonjwa mengi tu zaidi ya 72 yaliyo ndani ya miili
yetu.
Utafiti wa
kitaalam unaonyesha kuwa ndani ya zao la Tangawizi kuna vyanzo vikubwa
vya madini ya magenisium, manganese, Selenium, Iron, Vitamini B6 ambavyo
kwa pamoja huleta kinga tosha kwa baadhi ya maladhi ikiwemo maladhi ya
ngozi japokuwa wataalam wamethibitisha Tangawizi kuwa na msaada mkubwa
katika mwili wa binadamu kwa mmea huo kuwa na uwezo mkubwa katika kutibu
magonjwa mengi sana yanayotusumbua.
Yafuatayo ni baadhi ya magonjwa yanayoweza kutibiwa na tangawizi:-
Maumivu ya tumbo:Tangawizi inatumika kutuliza maumivu ya tumbo, yanayotokana na matatizo ya usagaji
chakula, kuharisha, kuvimbiwa, n.k. Inapotumiwa katika chakula
tangawizi husaidia usagaji chakula. Aidha tangawizi humuongezea mtu hamu
ya kula.
Matatizo ya Moyo: Tangawizi
hupunguza kiwango cha mafuta mwilini hivyo humsaidia na kumwepusha mtu
na matatizo ya moyo kwa kuyeyusha mafuta katika mishipa ya kusukuma
damu.
Matatizo ya Kupumua: Huondoa homa ya mafua, hutumika kutibu pumu, na pia kufungua mfumo wa upumuaji hasa inapotumika pamoja na asali.
Maumivu:uondoa maumivu ya misuli kwa sababu tangawizi ina uwezo mkubwa wa kulainisha misuli hasa pale inapopakwa sehemu iliyoathirika.
Maumivu ya Hedhi: Hupunguza maumivu ya wakati wa hedhi kwa wanawake.
Malaria: Husaidi kutibu Malaria na Homa ya Manjano.
Nguvu za Kiume: Tangawizi husaidia kuongeza nguvu za kiume kwa kutibu tatizo la mwanamume kutoa shahawa haraka.
Figo:Inaaminika kuwa tangawizi inatibu tatizo la vijiwe vya kwenye figo.
Saratani: Hutumiwa na wataalamu wa kimatibabu katika tiba ya saratani.
No comments:
Post a Comment