Zifahamu faida za kutumia kitunguu swaumu kama dawa.

 

 
Kitunguu Swaumu kama dawa


Kitunguu swaumu ni miongoni mwa viungo vinavyotegemewa katika kuongenza ladha nzuri kwenye vyakula mbalimbali, lakini wakati kiungo hicho kikitegemewa katika kuonogesha vyakula wataalam wa tiba asili wanasema ni kiungo hicho ni dawa endapo kikitumika vizuri.


Miongoni mwa magonjwa ambayo yanaweza kutibika kwa kutumia kitunguu swaumu ni pamoja na ugonjwa wa kifua, au mkamba, ambapo wataalam wa tiba asili wanasema kuwa, ugonjwa huo hujitokeza baada ya mifereji inayoingiza hewa mapafuni kupata maambukizi na kusababisha mgonjwa kukohoa kikohozi  mara kwa mara, huku kikiambatana na makohozi mazito. 

Ugonjwa mwingine ambao unaweza kutibiwa na kiungo hicho ni :-
kuharisha, hali kadhalika pia husadia kutibumishipa iliyovimba ambayo hujikunja na hivyo kusababisha maumivu makali sana na mara nyingine mishipa hiyo huonekata katika miguu ya watu wa makamo na akina mama wajawazito.Kitunguu swaumu pia hutibu aina mbalimbali za tambaza kama ya mifu, misuli na viungo pamoja na wale watu wenye matatizo ya kupata choo kwa muda wa siku mbili au zaidi anaweza kutibiwa kwa kutumia kitunguu swaumu.

Matumizi na maandalizi ya kitunguu swaumu katika tiba yanategemea aina ya maradhi unayotaka kuyatibu,hivyo basi ni muhimu kuwasiliana na wataalamu wa tiba mbadala ili uweze kupata maelekezo sahihi ya namna ya kuandaa kulingana na ugonjwa unaokusumbua.Kumbuka kama tulivyosema awali kuwa kitunguu swaumu kikipikwa kinapoteza nguvu ya tiba kutegemeana na tiba unayokusudia.

Kumbuka pia kwamba kitunguu swaumu huweza kuchanganywa na vitu vingine mfano;maziwa,asali,habatsouda,juisi,shayiri n.k.kutegemea na maradhi unayotaka kuyatibu na kwa ushauri/maelekezo ya daktari.

No comments:

Post a Comment