Maendeleo
ya sayansi na teknolojia yamebadili mfumo wa maisha ya watu pamoja na
kuathiri afya zao kwa kiasi kikubwa. Hivi leo watu wanatumia vyombo
mbalimbali vya usafiri kwenda karibu kila eneo.
Kwa hakika kutembea kwa miguu kuna manufaa mengi sana kwa ajili ya afya ya mwili, uchumi na maisha yako ya kijamii.
Ikiwa unapenda kuwa bora na mwenye tija zaidi katika nyanja zote, basi fahamu faida 25 za kutembea kwa miguu.
1. Hukabili maradhi ya moyo kwa kuhamasisha mzunguko mzuri wa damu.
2. Huimarisha mifupa.
3. Huondoa au kupunguza hatari ya kupata kiharusi.
4. Husaidia kupunguza uzito.
5. Huzuia saratani ya utumbo mpana.
6. Hukuwezesha kupata vitamini D kutoka kwenye jua.
7. Hukusaidia kuboresha usawa wa mwili wako (balance).
8.
Hukabili maradhi ya kisukari. Unapotembea unafanya mazoezi yanayoleta
uwiano wa urefu na uzito – BMI; jambo litakalokukinga na aina ya pili ya
kisukari (Type 2 Diabets).
9. Hukabili shinikizo la damu.
10. Huondoa msongo wa mawazo.
11. Huongeza utayari.
12. Hukufanya ujifunze mambo mbalimbali kwa kuona.
13. Hukuokolea gharama za nauli au mafuta.
14. Hupunguza lehemu mbaya mwilini (cholesterol)
15. Huimarisha misuli.
16. Husaidia mmeng’enyo wa chakula kwenda vizuri.
17. Huwezesha kinga mwili kujiimarisha na kujijenga (kutokana na sababu kuwa kutembea ni aina ya zoezi).
18. Huboresha uwezo wa kumbukumbu.
19. Hukujengea mahusiano ya kijamii. Unapotembea utakutana na watu mbalimbali.
20. Huzuia kuzeeka. Utafiti uliofanyika ulibaini kuwa watu wanaotembea umbali mrefu huishi zaidi.
21. Hukuweka katika hali nzuri (mood).
22. Hukusaidia kulala vizuri. Kumbuka mazoezi ni chanzo cha usingizi mzuri.
23. Huboresha afya ya uzazi hasa kwa wanaume. Kutembea kama zoezi ni njia ya kuwapa wanaume nguvu katika afya ya uzazi.
24.
Huzuia kuharibika kwa mimba. Mazoezi ni muhimu sana kwa mama mjamzito
kwa ajili ya afya yake na mtoto; hivyo zoezi rahisi na jepesi kwake ni
kutembea.
25.
Huboresha mwonekano wa mwili. Mazoezi ni njia moja wapo ya kuufanya
mwili wako uonekane katika umbo zuri. Hivyo kutembea kama aina mojawapo
ya zoezi kunaweza kukusaidia sana.
Neno la mwisho
Naamini umeona jinsi ambavyo kutembea kwa miguu kuna manufaa makubwa sana kwenye afya, uchumi na hata mahusiano yako ya kijamii.
Inashauriwa
kuhakikisha unatembea kwa miguu angalau dakika 30 kila siku. Kwa njia
hii utapata manufaa mengi yaliyotajwa hapo juu.
Je wewe huwa unatembea kwa miguu? Je kuna manufaa mengine unayoyapata?
No comments:
Post a Comment