"Kifo ni fumbo kubwa, tulizoea kumuona Dkt.Magufuli akiwa kwenye kile kiti nilichokaa Mimi, leo hatupo nae, Juzi ilinipa ugumu kutangaza kifo cha Rais wangu ila nikaambiwa hakuna mwingine wa kutangaza na leo tena nipo hapa huku Hayati Magufuli akiwa kwenye Jeneza.
Nilihusudu utendaji wa Hayati Magufuli tangu nikiwa Waziri, nilipenda michango yake Bungeni, alizijua Barabara zote za Nchi hii kwa majina na urefu wake, hakuogopa kutetea kilicho sahihi kwa maslahi ya Taifa, kwake saa 24 hazikumtosha kwenye kazi” Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
TAREHE 22/03/ 2021 DODOMA
No comments:
Post a Comment