Wanaume kabla ya kuoa huangalia mwanamke mwenye sifa hizi

 

 

 

 

Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa pamoja kwa kipindi chote cha maisha.

Wanawake wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachoweza kuwafanya wakapata wachumba ni uzuri hivyo kupoteza muda wao kujichubua na kujiremba ili wawavutie wanaume bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri.

Hali sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na sura nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za kuolewa.

Utafiti ambao nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa tabia na umbo, kuna kuna sifa nyingine za msingi ambazo mwanamke anatakiwa kuwa nazo ili aweze kuwa katika mazingira mazuri ya kupata mchumba wa kumuoa kiasi kwamba asipokuwa nazo ataishia kuchezewa tu lakini haitatokea mtu kumtakiwa kwamba anataka kumuoa.

1. Mwenye mapenzi ya kweli.

Lengo kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa mwanamke na ikiwezekana waweze kupata watotoa ambapo watoto hao ndio furaha ya ndoa. Wapo wanawake wengine ambao wanonesha wazi kutokuwa na mapenzi ya kweli bali wanakuwa na mapenzi ya kuzuga. Wanachotaka wao aidha kupata umaarufu tu kwamba yuko na mtu fulani ama kuweza kupata pesa alizonazo mwanaume lakini sio kwamba ana mapenzi ya dhati kutoka moyoni mwake.

Mwanamke asiye na mapenzi ya dhati utamgundua tu, muda mwingiutamuona macho yake yako kwenye mfuko wa mwanaume. Akiona kwamba mfuko umetuna utaona anaonesha mapenzi ya hali ya juu lakini pindi hali inapokuwa kubwa mbaya kifedha mapenzi yanaanza kufifia.

Kwanini wanaume wanapenda wana wake wenye mapenzi ya dhati kutoka mioyoni mwao na si kutokana na fedha walizonazo? Hii inatokana na ukweli kwamba maisha siku zote yanabadilika, kama waswahili wanavyosema, kuna kupanda na kushuka.

Sio kwamba kila siku utakuwa na maisha mazuri na kama itatokea hivyo basi ushukuru mungu.Hivyo basi mwanamke wa kuoa lazima afahamu hivyo na awe tayari kuonesha mapenzi yake ya dhati wakati wote wa maisha yao na si kwa kipindi fulani tu cha neema.

Si hivyo tu pia asilimia kubwa ya maisha ya ndoa yanatawaliwa na mapenzi, kwa hiyo nyanja hiyo inakuwa ya msingi sana kwa wanaume wengi kuiangalia ili wasije wakajikuta wanaoa mwanamke ambaye baada ya muda mapenzi yanakwenda likizo hali ambayo inaweza kuwafanya wasiishi maisha ya raha mustarehe.

2. Wenye tabia nzuri

Tabia njema ndio silaha ya maisha, ukiwa na tabia nzuri kila mtu atakupenda, hiyo ni katika maisha ya kawaida. Lakini linapokuja sualana kuoa tabia inakuwa kitu cha awali sana kungaliwa na hiyo inaweza kuwa na ukweli kwa sababu wapo wasichana wazuri wenye mvuto wa aina yake na maumbile mazuri, lakini wanakosa wanaume wa kuwaoa, ukiuliza kwani utaambiwa anatabia mbaya.

Naweza kusema hilo ndilo limekuwa tatizo kubwa kwa baadhi ya wanawake kukosa wanaume wa kuwaona. Hakuna mwanaume hata mmoja kati ya wale ambao nimejaribu kuongea naye ambaye ameonesha kulidharau suala hilo la tabia.

Si hivyo tu wapo wanaume ambao wameingia kichwa kichwa na kuoa kwa kuangalia sura tu bila kujali tabia, matokeo yake baada ya siku chache yanatokea machafuko ya aina yake hali ambayo imepelekea kuvunjika kwa ndoa kutokana na tabia mbaya alizonazo mwanamke.

3. Mwenye uchu wa maendeleo

Hivi karibuni kumekuwepo na mabadiliko ya aina yake kwa wanaume, wengi sasa hivi hawapendi kabisa kuoa mwanamke ambaye hana kazi yaani ‘golikipa’. Kama atakuwa hana kazi basi awe na uchu wa maendeleo kwa kujituma kufanya kazi mbalimbali za kimaendeleo kama vile kilimo kwa wale walio vijijini na biashara ndogondogo kwa wale ambao wako mijijini na hata vijijini.

Ile dhana ya kusema mwanamke ni mama wa nyumbani wa kukaa na kujipodoa akimsubiria mwnaume arudi amstarehesha, sasa hivi imepitwa na wakati. Wanaume wengi wanapenda wanawake ambao ni wahangaikaji, wenye ndoto za maendeleo katika maisha yao. Hata kama watakuwa si wafanyakazi lakini wawe wenye kutoa ushauri kwa waume zao juu ya jinsi gani wafanye ili wafanikiwe.

4. Wasiopenda makuu.

Kuna wanawake wengine wanakuwa na tabia za ajabu sana kiasi kwamba yaweza kuwa kero kwa wanaume. Wapo wanawake ambao wanapenda makuu bila kujali hali halisi ilivyo. Kuna wanawake naweza kusema wana tamaa, kila wikiendi utamsikia “leo tunakwenda wapi dear?”

Akimuona rafiki yake kanunua simuya laki tatu na yeye utamsikia akisema, ‘na mimi naomba uninunulie simu kama ya Grace’. Ukienda naye Pub anakuambia,”mimi sinywi pombe za chupa natumia za kopo tena Heineken’. Yeye hajali kiasi cha pesa mwanaume alicho nacho na usipotekelezea anachukia na anaweza hata kupunguza mapenzi.

Wanawake kama hawa wako katika mazingira magumu sana ya kuweza kupata wanaume wa kuwaoa. Mara nyingi katika maisha fedha huzungumza, kama mwanaume atakuwa na pesa ya kutosha itakuwa rahisi sana kwa mwanamke kupata kila atakachopenda lakini si kwa kumwambia mimi nataka kitu fulani.Mwanaune mwenyewe utamsikia akisema, ‘unataka nikununulie simu ya aina gani, au leo unataka twende wapi?’ hapo ndipo utakuwa na nafasi ya kusema, ‘mimi nataka uninunulie simu kama ya fulani ama leo nataka twende sehemu fulani.’

Wanaume ni warahisi sana wa kuwapatia wale ambao wanatarajia kuwaoa chochote ambacho watahitaji kama tu pesa haitakuwa tatizo. Kitu ambacho kinawaudhi wanaume wengi ni ile tabia ya mwanamke kupenda mambo makubwa bila kuangalia uwezo uliopo kwa mwanume.

Kuna wanawake wengine wao si wasemaji kabisa, yeye anasubiri leoamemletea hiki, anapokea na kushukuru, kesho akiambiwa twende beach anakubali. Au wengine wanasubiri mpaka waulizwe wanataka nini, ndio wanasema.

Sisemi kwamba uwe mkimya tu hata kama una shida ya kitu fulani na unafahamu kwamba ukimweleza mwenza wako anaweza kukusaidia, hapana! kama unaona kwamba uwezekano wa kupata kile ambacho unakihitajiupo mweleze kwa utaratibu naamini atakuelewa na kukutimizia.Tabia ambayo hawaipendi wanaume wengi ni ile ya kulazimisha ufanyiwe kitu fulaniwakati inawezekana uwezekano haupo.

5. Wavumilivu.

Wapo wanawake ambao sio wavumilivu kabisa katika maisha.Tunajua kwamba maisha siku zote hayatabiriki, yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama kifedha.Huu ndio wakati wa kuona uvumilivu wa mtu.Kama mwanamke anatarajia kwamba siku zote ni za raha tu na pindi matatizo yanapotokea anachukua uamuzi wa kumtoroka mwanume, huyo siyo mwanamke wa kuoa.

Wangapi leo hii huwatoroka waume zao pindi inapotokea kuumwa, kufilisika ama kupatwa na tatizo lolote ambalo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kuwafanya maisha yao kutingishika?

Uvumilivu kwa mwanamke utakuwepo kama tu atakuwa na mapenzi ya dhati kama nilivyozungumza hapo awali. Mwanamke mweye mapenzi ya dhati ni lazima atakuwa mvumilivu na atakuwa tayari kuishi katika maisha ya aina yoyote, yawe ya raha ama ya starehe.Hawa ndio wale ambao wanaume wengi wengependa kuwa nao maishani mwao.

Kwa maana hiyo basi hiyo iwe changamoto kwa wanawake. Wajue kwamba wanaume wanafurahi kuwa na wanawake wa aina gani. Hata kama utakuwa umeshaolewa, kama kuna wakati kunakuwa na kutokuelewana baina yenu, chunguza yawezekana kwamba unakosa mojawapo ya tabia ambazo nimezitaja hapo juu. Waweza kubadilika kwani inawezekana.

 

SOURCE MUUNGWANA BLOG 

Read More

Vyakula vya Kuepuka Kula kwa Wanaume

 

 Katika makala hii hii utajifunza vyakula mbalimbali ambavyo wanaume hawatakiwi kula ili kubaki na afya bora wakati wote. Kuna vingine unaweza kuwa unavitumia kila siku bila mwenyewe kujuwa.

Punguza kula vyakula feki kuzuia kupoteza nywele

Moja ya matatizo makubwa upande wa urembo kwa wanaume ni kupoteza nywele (upala). Lakini kama unatafuta kitu cha kukilaumu dhidi ya tatizo lako la kunyonyoka nywele basi ni hiyo sahani yako ya chipsi unayokula kila siku.  Vyakula feki (junk foods) ni hivyo vinapatikana kwenye fast foods na takeaway centers nyingi hasa mijini kadharika vyakula vile vyote vya kwenye maboksi.

Vyakula hivi feki vina kiasi kingi mno cha lehemu (cholesterol) na lehemu hii hupelekea kile huitwa kwa kitaalamu kama ‘pregnenolone’ na kupelekea kiasi kikubwa cha ‘dihydrotestosterone’ (DHT) na hatimaye kupotea kwa nywele kichwani a.k.a upara.
Kunyonyoka kwa nywele kunaweza kuwa ni jambo la kurithi (genetics) lakini vile vile aina ya chakula unachokula kinaweza kuwa kinahusika moja kwa moja.

Punguza kunywa pombe 
Wanaume wengi wanaokunywa bia kupita kiasi huwa na uwezekano mkubwa wa kupatwa na tatizo la kuota matiti kama wamama tatizo lijulikanalo kwa kitaalamu kama ‘gynecomastia’.

Kwenye bia au pombe mara nyingi hakuna lishe ya moja kwa moja na hivyo hukufanya ujisikie njaa au hata kuongzeka kwa njaa zaidi na ndiyo sababu unaambiwa kama huna uhakika utakula wapi ni bora usinywe pombe ili kulinda afya yako.

Kwenye bia kuna kitu kama homoni ya oestrogen ya kupandikizwa na hivyo unywaji pombe kupita kiasi kuna uhusiano wa moja kwa moja na matokeo ya wanaume kuwa na matiti kama wanawake.

Acha kutumia mafuta ya mboga mboga kuepuka saratani ya tezi dume
Mafuta yatokanayo na mboga mboga au mimea yamekuwa yakipigiwa debe kwa miaka mingi na watu wanaojihusisha na lishe na wale wenye hasira sana na mafuta yatokanayo na wanyama. Hata hivyo leo nakujulisha mafuta hayo si salama sana kutumika na mwanaume kila siku. Hili limekuja hasa kutokana na kuongezeka kwa magonjwa ya moyo na lehemu na watu walazishwawa kutumia mafuta ya namna hiyo.

Lakini mafuta haya ya mboga mboga ndiyo kitu kibovu kabisa unatakiwa kukiepuka ili usipatwe na saratani ya tezi dume.  Linapokuja suala la kujilinda saratani ya tezi dume basi mafuta yenye omega 3 ndiyo suluhisho la kudumu na siyo omega 6 kama ilivyo kwenye vyakula vingi vya kwenye makopo, mafuta ya alizeti, maharage ya soya, mafuta ya  canola na mafuta ya corn na mengine yote yenye omega 6.

Popcorn
Popcorn au bisi ni chakula kingine mwanaume hatakiwi kula, hupikwa kwa kutumia mafuta yasiyo na afya, sodiamu nyingi na ni chanzo cha baadhi ya kansa. Kuna kitu kinaitwa ‘Diacetyl’ kinachopatikana kwenye popcorn ambacho kinahusika na kusababisha kansa na kuna kingine kiitwacho ‘Perfluorochemicals’ ambacho huathiri tezi ya thyroid na ugonjwa wakati huo huo husababisha ugonjwa wa kupungukiwa umakini ujulikanao kwa kiingereza kama ‘Attention-deficit/hyperactivity disorder (ADHD)‘.Ni vizuri kuacha kula popcorn.

Mkate mweupe
Mkate mweupe una wanga mwingi zaidi usio na faida. Kwenye hatua za kutengeneza mkate mweupe vitamini zote za kundi B hupotea, hupotea pia nyuzinyuzi (fiber). Siyo hivyo tu mkate mweupe umesemekana kuwa ni sababu ya ugonjwa wa kisukari na kuongeza uzito zaidi mwilini wakati huo huo ukisababisha tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana.

Vingine vinavyofanana na na hilo ni ugali wa sembe, tambi nyeupe, chai ya rangi na kahawa. Kula mkate ambao ngano yake haikukobolewa (brown bread), kula ugali wa dona na chai unaweza kutumia tangawizi au mdalasini badala ya majani ya chai.

Chumvi ya mezani
Chumvi ya mezani ile ya unga nyeupe haifai kwa mwanaume. Kila mmoja amesikia chumvi hii husababisha shinikizo la juu la damu na pamoja na hayo bado sehemu kubwa ya watu wanatumia chumvi hii.

Chumvi ya mezani husafishwa kwa kuondoa madini, madini na hupitishwa katika joto la nyuzi joto. Kwa hiyo uliyonayo sasa ni asilimia 40 ya sodiamu na asilimia 60 ya kloridi, na kisha kemikali kama vile ‘aluminium silicate’ huongezwa ili kuifanya isishikane na hivyo kubaki katika hali ya unga. Aluminium silicate ni sumu kali inayoharibu mfumo wetu wa fahamu. Inatajwa kuwa ni miongoni mwa sababu zinazosababisha ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

Chumvi ya mawe ya baharini ile ambayo haijapita kiwandani (unrefined sea salt) ndiyo nzuri zaidi kwa afya ya mwanaume.

SOURCE, MUUNGWANA BLOG, 27/3/2021

 

Read More

Rais wa Jamhuri ya Watu wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta akitoa Heshima za Mwisho

  

 


Rais wa Jamhuri ya Watu wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta akitoa Heshima za Mwisho kuaga Mwili wa aliyekuwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Mazishi ya Kitaifa yaliyofanyika leo March 22,2021 katika Uwanja wa Jamhuri JIjini Dodoma.

Read More

Rais wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi akitoa Heshima za Mwisho kwa Mpendwa wetu Hayati Dkt Magufuri

  


 

 

Rais wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi akitoa Heshima za Mwisho kuaga Mwili wa aliyekuwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Mazishi ya Kitaifa yaliyofanyika leo March 22,2021 katika Uwanja wa Jamhuri JIjini Dodoma.

Read More

Maneno Machache ya Hotuba ya Rais Mama Samia Suluhu Hassan

 

 

"Kifo ni fumbo kubwa, tulizoea kumuona Dkt.Magufuli akiwa kwenye kile kiti nilichokaa Mimi, leo hatupo nae, Juzi ilinipa ugumu kutangaza kifo cha Rais wangu ila nikaambiwa hakuna mwingine wa kutangaza na leo tena nipo hapa huku Hayati Magufuli akiwa kwenye Jeneza. 
 
Nilihusudu utendaji wa Hayati Magufuli tangu nikiwa Waziri, nilipenda michango yake Bungeni, alizijua Barabara zote za Nchi hii kwa majina na urefu wake, hakuogopa kutetea kilicho sahihi kwa maslahi ya Taifa, kwake saa 24 hazikumtosha kwenye kazi” Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
TAREHE 22/03/ 2021 DODOMA
Read More

Picha Rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan. Mungu Akulinde Rais wetu

  


 

 

Picha Rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Mama Yetu Tunakupenda Sana, Mungu akupe nguvu ya kuendelea pale Baba Magufuri alipo achia.

Read More

Buriani Hayati DKT John Magufuri wana Katoro Geita na Chato Wanakulilia,

  

 


Citizens of Katoro Geita and Buseresere Chato standing on the road while others are putting cloth and cloth as a sign of respect to the former President of the Republic of Tanzania in the fifth term Hayati Dr. John Pombe Magufuli when he was passed to his home in Chato today 24th March 2021.

Read More

Wananchi wa Katoro Geita na Buseresere Chato Wakisimama Barabarani Kumuaga Hayati Rais Dkt John Pombe Magufuri

 

 

 


 

Wananchi wa Katoro Geita na Buseresere Chato wakiwa wamesimama barabarani huku wengine wakitandika kanga na nguo kama ishara ya Heshima ya kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli wakati akipitishwa kuelekea Nyumbani kwake Chato leo tarehe 24 Machi 2021.

Read More

Wasifu wa marehemu DKT John Pombe Magufuli

 


 

John Pombe Joseph Magufuli alikuwa rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Alichaguliwa Oktoba 2015 na kurithi mikoba ya Jakaya Mrisho Kikwete. Alikuwa mwanasiasa mwenye sifa ya uchapakazi na asiye na mazaha.

Matangazo ya kibiashara

Magufuli au JPM kama alivyofahamika, alichaguliwa kwa mara ya kwanza 1995 katika nafasi ya ubunge, na akahudumu katika baraza la mawaziri katika nafasi ya naibu waziri wa ujenzi kuanzia 1995 hadi 2000, waziri wa ujenzi kuanzia 2000 hadi 2006, waziri wa ardhi na maendeleo ya makaazi mwaka 2006 hadi 2008, na waziri wa ujenzi kwa mara ya pili kuanzia 2010 hadi 2015. Akisimama kama mgombea wa chama tawala - Chama cha Mapinduzi CCM, alishinda uchaguzi wa mwaka 2015 kwa kura 8,882,935 na aliapishwa Novemba 5, 2015 kuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akilihutubia taifa usiku wa Februari 17, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alisema Magufuli alifariki majira ya saa 12:00 jioni kutokana na tatizo la moyo.

Amesema kwamba rais Magufuli aliaga dunia katika hospitali ya Mzena iliyopo jijini Dar es Salam mwendo wa saa kumi na mbili jioni saa za Afrika Mashariki kutokana na matatizo ya moyo.

Kwa mujibu wa makamu huyo wa rais Magufuli alikuwa chini ya uangalizi wa madaktari wa moyo kutoka hospitali ya Jakaya Kikwete.

 

Read More

Anna Tusajigwe Mwakasege, Ni Rubani aliyeuaminiwa kuendesha ndege iliyobeba mwili wa Rais Hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuri

 


Huyu ni mmoja wa marubani wawili waliorusha ndege iliyobeba mwili wa Rais Magufuli. Anaitwa Anna Tusajigwe Mwakasege. Ni binti wa pili wa Mwalimu Christopher na mama Diana Mwakasege.
Anna alipata maono ya kuwa rubani akiwa darasa la 3 tu. Baba yake akampeleka uwanja wa ndege angalau kuona ndege "live" badala tu ya kuziona angani tu. Alipofika darasa la 5 baba yake alitembeza uwanja mdogo wa ndege Arusha ambapo alipata nafasi ya kuongea na marubani kuhusu ndoto yake, nao wakampa ushauri masomo ya kusoma ili aweze kuifikia ndoto hiyo.
Alijifunza urubani Afrika kusini, na siku anarusha ndege kwa mara ya kwanza baba yake hakulala usiku huo (hii ni story ya wakati mwingine).
Lakini kwa sasa Anna ni miongoni mwa marubani wa shirika la ndege ATCL. Kabla ya kujiunga na ATCL alifanya kazi mashirika mengine makubwa ya ndwge kama SAA na kupata uzoefu wa kuendesha ndege kubwa kama Boeing 747, Boeing 777 na Airbus A340.
Hongera
Anna kwa kuaminiwa kuendesha ndege iliyobeba mwili wa Rais. Umeweka alama kubwa kwa taifa hili, ambayo haitafutika kirahisi. Mara zote tutakapokumbuka kifo cha JPM tutakumbuka kuwa wewe kama Senior First officer na rubani mwenzio (kiongozi) ndio mlipata neema ya kubeba mwili wake.
Najua si kazi rahisi kuendesha ndege ukiwa na majonzi ya kumpoteza Rais wako lakini umeaminiwa na umeweza. Tunawaombea kwa safari ya Zanzibar, Mwanza na Chato. Wewe pamoja na cabin crew yote. Hakika wanawake mnaweza. Unaweza kumfollow kule Instagram kwa kuandika @tusajigwe01 @tusajigwe01 #TheFutureIsFemale #WomenEmpowerment #WanawakeWanaweza
 
SOURCE FROM FACEBOOK - ACCOUNT 
Malisa GJ


Read More

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli - Tutakukumbuka Baba kwa Mengi Uliyoyafanya Mazuri

 

 

 


 

Ndugu John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Umevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo umeumaliza, Imani Umeilinda. 
 
Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa Jina lake Lihimidiwe. Amina!
Read More

Mama Samia Suluhu Hassan Kuwa Mrithi wa Rais John Pombe Magufuri

 

 
 

Mama Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa Makamu wa Rais toka mwaka 2015 sasa atakuwa mrithi wa rais John Magufuli ambaye amefariki jana Jumatano Machi 17.
Samia atashikilia wadhifa huo kwa kipindi kilichosalia cha cha muhula wa urais mpaka 2025, kwa mujibu wa katiba ya Tanzania.
 
Anatarajiwa kuweka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo wa juu zaidi nchini Tanzania. Pia atakuwa rais wa pili wa Tanzania kutokea Zanzibar, wa kwanza akiwa Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyeliongoza taifa hilo kwa miaka 10 kutoka mwaka 1985 mpaka 1995.
 
Read More

Yesu Alivumilia hadi Mwisho

 





Yesu Alivumilia majaribu, mateso, dhabihu, na dhiki za Gethsemani, pamoja na kuteseka kwake kule Golgotha msalabani. Kisha, hatimaye, Aliweza Kusema, Imekwisha (Yohana 19:30). Alikuwa amekamilisha kazi Yake akiwa katika hali ya mauti na kuvumilia hadi mwisho, hivyo basi kukamilisha dhabihu ya kulipia dhambi.

Katika bustani Alisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe. (Mathayo 26:39).

Katika Mafundisho na Maagano tunafundishwa:

Mateso ambayo yalisababisha Mimi mwenyewe, hata Mungu, mkuu kuliko wote, kutetemeka kwa sababu ya maumivu, na kutoka damu kwenye kila kinyweleo, na kuteseka mwili na roho—na kutamani nisinywe kikombe kichungu, na kusita—

Hata hivyo, utukufu na uwe kwa Baba, na Mimi nikachukua na kukamilisha maandalizi yangu kwa wanadamu” (M&M 19:18–19).

Yesu Alimwambia Baba Yake, “Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye” (Yohana 17:4).

Kisha, msalabani, “basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, Imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake” (Yohana 19:30).

Yesu alikuja duniani, akasalia na Uungu Wake ili Yeye aweze kutekeleza ile dhabihu ya kulipia dhambi, na kuvumilia hadi mwisho.

Read More

Yesu Alikuwa na Sifa za Kipekee

 



 Ni Yesu Kristo pekee ambaye angeweza kutekeleza dhabihu ya kulipia dhambi—akiwa amezaliwa na mama mwanadamu, Maria, na akiwa amepokea nguvu za uzima kutoka kwa Baba Yake (ona Yohana 5:26). Kwa sababu ya nguvu hizi za uzima, Alishinda mauti, nguvu za kaburi zilibatilishwa, na akawa Mwokozi na Mpatanishi na Bwana wa Ufufuko—njia ambayo kwayo tunapata wokovu na uwezo wetu sisi sote wa kuishi milele. Tutafufuliwa na kuishi milele kwa sababu ya dhabihu ya Yesu Kristo ya kulipia dhambi.

Read More