(OFFICIAL VIDEO) Angel Benard – ASANTE

Share it Please

 






"AMEANDIKA ANGEL BERNAD JUU YA WIMBO WAKE MPYA"


Nimeandika huu wimbo kama ishara ya shukurani kwa Mungu. Nimemuona Mungu akinitetea sana katika safari ya maisha ambayo amenipa. 
Mwaka 2006 nilifanya album iliyoitwa Yote Yalikwissha, 2010 nilifanya album inayoitwa Nakuabudu Milele, na Mwaka 2015 nilifanya album ya New Day na 2016 nikafanya Amplified Version ya album hiyo ya New Day. 
Utagundua kumekuwa na album mpya kila baada ya Miaka 5. 

Kila season imekuwa na madarasa mengi ambayo maneno hayatoshi kuelezea mambo ambayo Mungu amekuwa akifanya. 
Katika maandalizi ya Album hii ya Tano inayoitwa Turning around. Nilisikia msukumo wa kusema ASANTE kwa MUNGU. 
Ninaamini kila m moja ana kila sababu ya Kumshukuru Mungu. Hasa baada ya pito lililotishia dunia (covid).
 TUMEUONA MKONO WA MUNGU.

Binafsi NIMEMUONA MUNGU  akiniponya na magonjwa, na vita na mipango mingi ya kuzimu. Neema yake PEKEE IMETUWEKA HAPA TULIPO. 
Kama sio Bwana na tuseme Leo. 

Sijui kwa nini imempendeza Mungu kututunzia uhai huu aliotupa. Lakini jambo moja ninalojua ni kwamba, MAKUSUDI YAKE MAKAMILIFU NI LAZIMA YATIMIE. HATUPO HAPA KWA BAHATI MBAYA. TUPO KATIKA MIKONO SALAMA.

Zaburi 100:4
Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru;
Nyuani mwake kwa kusifu ; Mshukuruni,
lihimidi jina lake.

Kwa kuwa Bwana ndiye mwema; Rehema zake ni za milele;
Na uaminifu wake vizazi na vizazi.

Ndugu yangu. 
AKILI ZETU ZINA KIKOMO, LAKINI SIO MUNGU. 
ILIMRADI BADO YUPO ENZINI, BADO KUNA TUMAINI.

Mungu akubariki sana. 



No comments:

Post a Comment