BWANA YESU atukuzwe ndugu.
Karibu tujifunze mambo mazuri ya kutusaidia katika maisha yetu.Leo nazungumzia vijana na ujana.
Mapema kabisa Biblia inawashauri vijana kumcha MUNGU tangu ujana wao.Mhubiri 12:1 '' Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo. ''
Ni muhimu sana kwa kijana kumcha BWANA tangu mapema kabisa katika umri wake maana Kijana Asiyezoea Kujizuia Kimwili Kabla Ya Ndoa, Hataweza Kujizuia Katika Ndoa. Wasaliti Wengi Wa Ndoa Zao Ni Wale Ambao Hata Kabla Ya Ndoa Walishindwa Kujizuia Miili Yao Na Kuwapelekea Kufanya Uasherati. 2 Timotheo 2:22 '' Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao BWANA kwa moyo safi. ''
Baada ya kijana kumkumbuka MUNGU kwa kumpokea YESU na kuanza kuishi maisha ya Wokovu, Biblia inashauri kijana kuanza kuliishi neno la MUNGU, Kulifanya taa ya miguu Neno ili limuongoze kijana katika matendo mema na kumtii MUNGU siku zote. Zaburi 119:105 '' Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu. '' . Neno la MUNGU likiwa muongozo kwa maisha ya kijana kutakua na ushindi mkubwa sana kwa kijana huyo. Njia ya maisha ya kijana lazima iwe safi ndipo atampendeza MUNGU, Njia itakuwa salama kwa kijana kulitii tu neno la MUNGU(Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.-Zaburi 119-9)
Tena Wana Amani Nyingi Wasiokwazwa Na Maonyo Ya Neno La MUNGU (Zaburi 119:165, Wana amani nyingi waipendao sheria yako, Wala hawana la kuwakwaza. ).
Vijana wengi huwaza jinsi watakavyoingia kwenye ndoa, ushauri wangu ni huu Ukitaka Kujiweka Tayari Kwa Ndoa, Jiweke Tayari Kwa Upendo Wa Dhati, Usivutwe Na Vinavyoonekana Ambavyo Ipo Siku Havitakuwepo Au Vitapungua Au Vitapungua Uzuri Kwa Kukaa Mkao Ambao Wewe Huutaki.
-Binti Usitake Kuolewa Na Mwanaume Tu Mwenye Kipara Huku Moyoni Ukiamini Wenye Vipara Ndio Wenye Pesa Na Elimu Nzuri. -Kijana Wa Kiume Usitake Tu Kuoa Msichana Anayetoka Familia Ya Kitajiri Huku Ukiamini Moyoni Mwako Kwamba Utapata Sehemu Ya Urithi Ule.
Mke/mme Mwema Hapatikani Katika Mawazo Kama Hayo. Biblia Inasema " Upendelea Hudanganya, Na Uzuri Ni Ubatili; Bali Mwanamke Amchaye BWANA, Ndiye Atakayesifiwa-Mithali 31:30".
Biblia Hapo Ilipotaja Sifa Za Mke Mwema, Na Mme Mwema Ni Zilezile. Na Sehemu Nyingine Inauliza "Mke Mwema, Ni Nani Awezaye Kumwona?-Mithali 31:10a"
Na Biblia Kwa Kutusaidia Inajibu Yenyewe. Mithali 19:14b "Mke Mwenye Busara, Mtu Hupewa Na BWANA". Ndugu Zangu Mme/mke Mwema Hutoka Kwa MUNGU. Tafakari Na Chukua Hatua Za Utakatifu.
Vijana, ni jambo jema sana kumtii MUNGU.
Vijana wengi wamekufa mapema kwa sababu ya ukimwi na wengine wamejinyonga kwa sababu ya kusalitiwa na hiyo yote inasababishwa na kuingia katika mahusiano muda usio sahihi na ni matokeo ya kutokumtii MUNGU BABA.
Zaburi 32:1 ''Heri aliyesamehewa dhambi, Na kusitiriwa makosa yake. ''
MUNGU anapokutaka kijana umkumbuke wakati wa ujana wako ni kwa lengo tu la kukusaidia wewe.
-wamama wengi waheharibu wakati wa ujana wao na kupelekea kutokuolewa maisha yao yote.
-Wamama wengi walizalishwa wakati wa ubinti wao na kupelea leo hakuna anayejitokeza kuwaoa.
- Mabinti leo wengi kutoa mimba imekuwa kama tu kujisaidia haja kubwa, ni hatari sana.
-Kizazi kinaangamia kwa sababu ya vijana kutokumcha BWANA.
Vijana wengi hupanga kuutumia ujana wao kwa shetani ili waje wautumie uzee wao kwa MUNGU, ndugu zangu sio wote wanaofika uzeeni na hata wengi walio kuzimu ni kwa sababu walikuwa na mawazo kama hayo. 1 Yohana 3:8-10 '' atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa MUNGU alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. Kila mtu aliyezaliwa na MUNGU hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na MUNGU. Katika hili watoto wa MUNGU ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na MUNGU, wala yeye asiyempenda ndugu yake. ''
BWANA YESU anataka kuutumia ujana wako kwa mambo ya ulinzi na uzima lakini na shetani naye anataka autumie ujana wako ili kukuangamiza. Ndugu kijana usikubali kumfuata shetani bali jiunganishe na uzima kwa kumpokea BWANA YESU na kuliishi neno la MUNGU.
Vijana ni watu muhimu kwenye ufalme wa MUNGU.
Mtii MUNGU na kumtumikia wakati wa ujana wako.
Kataa dhambi, ogopa dhambi , ikimbie dhambi na usitende dhambi.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
No comments:
Post a Comment