KUFUNGWA USIONE NAFASI

Share it Please

 





Na Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima , Ufufuo na uzima


Kuna uwezekano wa mtu kufungwa asione nafasi (opportunities) ambayo Mungu amempa kwaajili ya mafanikio yake. Shetani anaweza kumfunga mtu ili asione nafasi ya mafanikio yake.

Siku moja nilialikwa na mtu mmoja mwenye ofisi kubwa ili kuwashauri watu fulani. Nikiwa ofisini nikakutana na secretary wake. Chaajabu yule secretary aliniona Nikiwa na t-shirt yangu akaniambia nikae nje; hakutaka hata nionane na bosi wake. Baada ya muda yule mtu akampigia secretary kumuuliza kuwa ""baba" amefika ofisini?" ndipo yule secretary alipofahamu kuwa hata bosi wake ananiita baba.

Alishtuka sana na kuanza kuomba msamaha. Tatizo la yule secretary ni kwamba alifungwa asinijue. Nafasi uliyonayo, elimu au Shetani anaweza kukuficha usione nafasi ambayo Mungu amekupa Katika maisha yako.

Katika Jina la Yesu nakuweka huru kutoka Katika vifungo vya kutoona Katika Jina la Yesu.
- Mch. Josephat Gwajima

No comments:

Post a Comment