ISHI UALISIA WAKO, ACHA KUISHI MAISHA YA ARTIFICIAL, JIFUNZE KUISHI KWA UTOSHELEVU:

Share it Please

 













Na Mtume na Nabii: Josephat Elias Mwingira


Unakuta mtu mfano anaishi Manzese, nyumba ya kupanga, anafunga ndoa, akimaliza eti anaenda Honyemoon, kwenye chumba cha Hotel, eti mnalala kwenye Viyoyozi (Air condition) wakati nyumbani kwako hata Pangaboi hakuna.
Mimi nilipoa nilimpeleka moja kwa moja Mke wangu Mahali nilipokuwa naishi ambapo hakuna Pangaboi ili aendelee Kufuta Jasho tangu Mwanzo, Si alinipenda mwenyewe, Sasa Maisha ya ARTIFICIAL NILIKATAA, Siwezi Mimi kutoka Harusini tumevaa tumemeremeta…. Honeymoon Kempensik, unamaliza Honeymoon sijui ni Silversand au Whitesand, unalala unapunga Upepo, watu (wahudumu wa hotel) wanawatumikia, unashika mkeo unatembea kwenye Mchanga, unakaa kule siku mbili tatu Honeymoon, siku ya Tatu unabebwa na Taxi unarudi nyumbani kwako …… Manzese (mahali pako pa Asili ambapo unaishi, sio kama kule Honeymoon ambapo kulikuwa na Viyoyozi (Air condition), Unahudumiwa n.k…..Wakati kwako huku hata Viyoyozi huna, hata Upepo wa Kupunga huna…… Hayo ni MAISHA YA ARTIFICIAL, Niliyakataa. Nilipofunga Harusi nilimchukua Mke wangu Moja kwa moja mahali nilipokuwa Naishi, ambapo hata pangaboi (feni) kulikuwa hakuna ili aendelee kufuta Jasho toka Mwanzo.
Na si ajabu sasa baada ya Kuoa mkaona pale Manzese kuna kelele nyingi Mkaamua kuhamia Buguruni kwenye Vyoo vya gorofa, Unampandisha hapo Mke wako, …. Sasa MMETOKA kule HOTELINI HONEYMOON kwenye Choo cha Kukaa cha Kuflash sasa unampandisha Mke wako kwenye choo cha kufunika na kitenge, tena cha kulenga

Nilikaa na Mpenzi wangu (Mke wangu) nakumwambia “Mke wangu hata tutakuwa hatuna Chakula, USIENDE KUOMBA, hata Kiberiti cha kuwashia jiko lako kwa Jirani”. Nikamwambia Mama tujifunze TUISHI kwa Kuangalia KRISTO Ametupatia kitu gani, ili Moyo wangu USISHIKWE na Uudunia, USISHIKWE na Wanadamu. Kwa hiyo tuliishi Mke wangu hakuweza hata kwenda kwa Jirani kuomba kiberiti cha Kuwashia jiko mpaka leo, Hajawahi kwenda kwa jirani kumwambia Naomba nichukue Kaa la Moto niliweke hapa kwenye Jiko langu Nikolezee Moto, Na hata siku tulipooana SIKUMPELEKA Mke wangu kwenye Chumba cha Hoteli “Honeymoon” eti mnalala kwenye Viyoyozi (Air condition) wakati Nyumbani kwangu hakuna hata Pangaboi (Feni), Nilimpeleka moja kwa moja Mahali nilipokuwa naishi ambapo hakuna Pangaboi ili aendelee Kufuta Jasho tangu Mwanzo.
NILIPOOKOKA Nikaazimia Moyoni mwangu “KWENDA VILE MUNGU Anavyonijalia”, Sikutaka KUHESABU Maisha ya Wengine yalivyo Bora niyajumlishe na ya Kwangu, Hapana,….. Hatukuzaliwa Nyumba moja, hata kama tulizaliwa Nyumba moja, tulipishana SIKU. Bahati nzuri sana Mimi ni Mtoto wa Mwisho Nayabeba ya Mwisho, kwa hiyo Nikakaa na Kukubali niwe wa Mwisho kama Nilivyozaliwa wa Mwisho ili YEYE ANITOE kule Mwisho ANIPELEKE MWANZO, Haleluyaaaa,….. Mwambie Mwenzako “HEBU ONDOKA kwenye Maisha ya ARTIFICIAL” 


Kuna wengi hapa mko sasa hivi Mnasomesha Watoto International School kwa MIKOPO…… UJINGA. Unaweka DENI kwa huyo Mtoto mpaka siku Anamaliza anakaa huku Kichwani KUNAMFUNDISHA Madeni, kwa hiyo, na yeye ataenda KUKOPA huko na huko, Atakopa watu, atakopa kule,…. HALIPI, siku ya kwenda MBINGUNI Aanazuiliwa MLANGONI, Kamalize Madeni Duniani.
Nilisema HAKUNA Mtoto wa Kwangu atakayesoma kwa Mkopo, NILIKATAA toka Mwanzo. NILIKATAA Mke wangu HATAVAA Nguo ya Mkopo eti nilipe Mwezi Ujao, HAKUNA, ….Hakuna Siku Mke wangu alichukua Kitenge cha Mtu au Kitambaa cha Mtu eti Alipe Mwezi Ujao, HAKUNA, Unaweza kumuuliza, Hakuna.
NILIKATAA toka Mwanzo, Nilisema MARUFUKU Kukopa. Nilimwambia Mama Vaa hayo Marapurapu SIKU Inakuja MUNGU ATABADILISHA,………. na Kweli MUNGU AMEBADILISHA Haleluya, Sasa hivi Yeye ndiye anachagua, mara leo Amevaa hivi, mara amevaa hivi. Nilimfundisha Mke wangu toka Mwanzo Kutosheka na kile Tulichonacho Muda huo, ili Moyo wangu USISHIKWE na Uudunia, USISHIKWE na Wanadamu. Haleluya, MUNGU ni MZURIIIIIIIIIIIIIII.
JIFUNZE KUISHI KWA UTOSHELEVU.
- Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

No comments:

Post a Comment