Muungano wa Maaskofu zaidi ya 15 na Wachungaji 100 mwanzoni mwa juma walizindua kitabu kinachoelezea uongozi uliotukuka wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
Kitabu hicho kimeandikwa na Mtendakazi katika shamba la Bwana, Restoration Bible Church Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Uzinduzi wa kitabu hicho kiitwacho Uongozi Uliotukuka, JPM ni Kiongozi wa Kisiasa na Kiroho, uliofanyika jijini Dar es Salaam uliongozwa na Askofu Mkuu wa Makanisa ya Naioth Gospel Assemblies of God ambaye pia ni katibu Mkuu mstaafu wa Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Tanzania, Dkt. David Mwasota.
Mwasota alisema lengo la kuandikwa kitabu hicho ni kutazama uongozi wa Rais Magufuli kwa pande za kisiasa na kiroho.
Askofu huyo alisema katika utendaji kazi wake, Magufuli anamtegemea Mungu hivyo kumfanya aonekane anaiongoza nchi kwa upande wa kiroho.
“Imani ya Mheshimiwa
Magufuli katika kushughulikia janga la Corona kiroho limefanya kuinua imani ya
watu wengi kwa kulisaidia kanisa ambalo ndiyo kazi yake kubwa kuwajenga watu
kiimani,” alisema askofu huyo.
-
Mwasota aliwaomba
maaskofu, wachungaji na waumini wote kuendelea kumuombea Rais Magufuli kwani
ndiyo yalikuwa maombi yao kwa miaka mingi kwa Mungu atuletee kiongozi kama
yeye.
No comments:
Post a Comment