NI MUNGU PEKEE NDIYE ANAYEDUMU MILELE

Share it Please

 






Mfanye Mungu awe kila kitu katika Maisha yako wala usizipe nafasi changamoto maana Mungu uliyenaye ni Mkubwa kuliko hizo changamoto.
Wakati mwingine changamoto zipo na ni nyingi sana na haujui hata ufanye nini, inafika mahali unakata tamaa kwa maana hauoni njia ya kutoka; Mwanangu usizitazame hizo changamoto zitatoweka, hakuna changamoto zinazodumu milele bali ni za kitambo tu, NI MUNGU PEKEE NDIYE ANAYEDUMU MILELE muangalie YEYE, mruhusu awe na wewe wakati wote na Tumaini lako uweke kwake hakika atakuvusha salama.
Zaburi 121:1-3 “Nitayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi? Msaada wangu u katika BWANA, Aliyezifanya mbingu na nchi. Asiuache mguu wako usogezwe; Asisinzie akulindaye;”
© MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA – KANISA LA EFATHA.

No comments:

Post a Comment