Mwelekeo Mpya wa FPCT Tanzania

Share it Please

 



Katika awamu ya tano  ya  Kanisa  la FPCT  chini ya  uongozi wa Askofu Mkuu , Mch Stevie Mulenga, Mungu ametupa neema ya mwelekeo au dira  inayofahamika kama  4U. Lengo  kubwa  likiwa kusimamia  katiba yetu, kurahisisha utekelezaji wa mpango mkakati wa FPCT  wa miaka 10 pamoja  na  miongozo  na sera  mbalimbali  za uendeshaji  wa  shughuli  za  kila  siku  ndani  ya kanisa FPCT. Mpango  huu  unasisitiza  na kuhamasisha  mambo  yafuatayo;

Uinjilisti  na Umisheni

Uwajibikaji  na  Uwajibishwaji,

Uchumi  na  Uchangiaji,

Uadilifu  na Uaminifu

4U kama  linavyotamkwa  katika  lugha  ya  kiingereza  linaweza  kumaanisha”For You” linamaanisha  “Ya kwako”.Yaani  mpangp  huu  ni  wa  kwako  na  hasa  kwa  mwana FPCT au mdau  yeyote wa kanisa  hili.Haya  mambo  yanayohamasishwa  na uongozi  mkuu  wa kanisa  ni  ya kwako si  ya  mtu  mwingine. kwa  hiyo  basi  tukizungumzia  Uinjilisti  na Umisheni  ni  wa  kwako  si wa mtu  mwingine,mtu  mwingine  anaweza  kuja  kuuunga  mkono  juhudi  za kwako  ambazo  zinaendelea  na hata  akiondoka  kwa sababu  ni ya  kwako  basi  wewe  unaendelea. Tunapozungumzia Uwajibikaji  na  Uwajibishwaji  nao  ni wa kwako  si  wa  mtu  mwingine   anayepaswa  kuwajibika  katika  eneo  lako  kama  kiongozi  wa  kanisa  ngazi  yoyote, kiongozi  wa  idara  au  taasisi  uwajibikaji  ni  wa kwako. Uadilifu  na Uaminifu   si  jambo  la  jumla lazima aanze  mtu  mmoja  na  kuwa  kielelezo  kwa watu  wengine. Katika  Uchumi  na Uchangiaji hii  nayo  ni  ya  kwako, mchangiaji si  mtu  kutoka  nje  ya kanisa letu, kama  atakuja  mtu  wa  nje  atakuwa  wa msimu  au  vipindi  Fulani  lakini  hii  ni  ya  kwako [For You]. Kimsingi  wote  tunakubaliana  kuwa  kitu  cha  kwako  lazima  ukijali, ukitunze, ukiboreshe, ukigharimikie, ukipende, ukipe  kipaumbele.

(ARTICLE FROM FPCT WEBSITE,2020)

No comments:

Post a Comment