Mama mzazi wa mcheza sinema maarufu wa Hollywood, Sylvester Stallone aka Rambo, Jackie Stallone, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 98.
Kupitia ukurasa wake wa twitter, mwanaye mdogo Frank Stallone ameandika kuwa mama yao huyo amefariki akiwa usingizini na kuongeza kuwa wamepokea kifo hicho kwa uchungu na maumivu makubwa.
“Asubuhi ya leo, kaka zangu na mimi tumempoteza mama yetu Jackie Stallone. Aliyekuwa mama wa watoto wanne, Tommy, Sylvester, Frankie na marehemu dada yetu Toni Ann.” aliandika Frank mdogo wake Sylvester.
Katika Twitter hiyo, Frank ameongeza kuwa, mama yao alikuwa mchapakazi na mwenye kupenda usawa na aliwalea vyema licha ya kuondokewa na mumewe ambaye aliwazaa yeye na kaka yake Sylvester aliyekuwa mwanasheria tajiri na kisha kuolewa tena.
Mama wa mcheza sinema huyo maarufu, alizaliwa Novemba 29, 1921 huko Washington DC na ameacha wajukuu Saba na vitukuu Watatu.
Muda wa maisha yake, kwa mujibu wa Frank, kaka yake Sylvester alikuwa akimlea mwanamke huyo kama malkia.
No comments:
Post a Comment