Moja ya kanisa linalotajwa kuwa la kale zaidi wilayani Rungwe. Kanisa hili linapatikana kijiji cha Ndubi/ Kisa, Kata ya Kisondela .
Katika awamu ya tano ya Kanisa la FPCT chini ya uongozi wa Askofu Mkuu , Mch Stevie Mulenga, Mungu ametupa neema ya mwelekeo au dira inayofahamika kama 4U. Lengo kubwa likiwa kusimamia katiba yetu, kurahisisha utekelezaji wa mpango mkakati wa FPCT wa miaka 10 pamoja na miongozo na sera mbalimbali za uendeshaji wa shughuli za kila siku ndani ya kanisa FPCT. Mpango huu unasisitiza na kuhamasisha mambo yafuatayo;
Uinjilisti na Umisheni
Uwajibikaji na Uwajibishwaji,
Uchumi na Uchangiaji,
Uadilifu na Uaminifu
4U kama linavyotamkwa katika lugha ya kiingereza linaweza kumaanisha”For You” linamaanisha “Ya kwako”.Yaani mpangp huu ni wa kwako na hasa kwa mwana FPCT au mdau yeyote wa kanisa hili.Haya mambo yanayohamasishwa na uongozi mkuu wa kanisa ni ya kwako si ya mtu mwingine. kwa hiyo basi tukizungumzia Uinjilisti na Umisheni ni wa kwako si wa mtu mwingine,mtu mwingine anaweza kuja kuuunga mkono juhudi za kwako ambazo zinaendelea na hata akiondoka kwa sababu ni ya kwako basi wewe unaendelea. Tunapozungumzia Uwajibikaji na Uwajibishwaji nao ni wa kwako si wa mtu mwingine anayepaswa kuwajibika katika eneo lako kama kiongozi wa kanisa ngazi yoyote, kiongozi wa idara au taasisi uwajibikaji ni wa kwako. Uadilifu na Uaminifu si jambo la jumla lazima aanze mtu mmoja na kuwa kielelezo kwa watu wengine. Katika Uchumi na Uchangiaji hii nayo ni ya kwako, mchangiaji si mtu kutoka nje ya kanisa letu, kama atakuja mtu wa nje atakuwa wa msimu au vipindi Fulani lakini hii ni ya kwako [For You]. Kimsingi wote tunakubaliana kuwa kitu cha kwako lazima ukijali, ukitunze, ukiboreshe, ukigharimikie, ukipende, ukipe kipaumbele.
(ARTICLE FROM FPCT WEBSITE,2020)