TANGAZO LA NAFASI YA KAZI – KATIBU MKUU WA DAYOSISI MASHARIKI NA PWANI

  

 


 

Kanisa La Kiinjili La Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP) ni miongoni mwa Dayosisi za KKKT. Dayosisi inaongozwa kwa mujibu wa Sheria za nchi na inakatiba yake ambayo imerekebishwa mwaka 2016.

Kwa mujibu wa Mpango Mkakati wa DMP wa Mwaka 2018 -2022 DMP ina Njozi, Utume, Tunu na Wito ambavyo vinapaswa kusimamiwa kama taasisi. Kwa kuzingatia haya yote hapo juu, DMP inatangaza nafasi ya Kazi ya Katibu Mkuu wa Dayosisi. Dayosisi inakaribisha maombi kwa mtu yeyote mwenye sifa za kuwa Katibu Mkuu kwa kufuata sifa zilizo ainishwa hapo chini.

CHEO/WADHIFA : KATIBU MKUU

Majukumu /Madaraka ya kazi.

  • Ataratibu na kusimamia utendaji wa watumishi wote wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP) isipokuwa Askofu na Msaidizi wa Askofu
  • Ataratibu na kusimamia masuala yote yanayohusu mali za Dayosisi, mapato, matumizi na miradi ya Dayosisi
  • Atakuwa ndiye mwajiri wa watumishi wote wa Dayosisi katika ngazi ya Mtaa, Usharika, Jimbo, Vituo vya Dayosisi na Ofisi Kuu ya Dayosisi kwa niaba ya Halmashauri Kuu

 

Uwajibikaji.

  • Atawajibika kwa Askofu wa DMP
  • Atashirikiana na Wakuu wa Idara, vitengo na Asasi kuhusu masuala ya usimamizi wa fedha

 

Majukumu muhimu.

  • Ni Mtendaji Mkuu wa mambo yote ya utawala na kwa hiyo atasimamia utekelezaji wa maamuzi ya vikao vya juu na maelekezo halali ya Askofu na Msaidizi wa Askofu;
  • Atakuwa kiongozi wa Manaibu Katibu Mkuu;
  • Katibu Mkuu kama kiongozi anatazamiwa awe tayari kukaribisha na kupokea mawaidha na ushauri na pia kutoa mapendekezo na kushauriana na Manaibu Katibu Mkuu ambao kwa nyadhifa zao wana fursa ya kuwasiliana na Katibu Mkuu moja kwa moja bila kupitia kwa mtu mwingine;
  • Atasimamia uandishi na usambazaji wa Mihutasari ya Mkutano Mkuu, Halmashauri Kuu, Halmashauri ya Utendaji kwa kufuata utaratibu uliowekwa au kama atakavyoagizwa na Halmashauri Kuu;
  • Kuongoza watumishi wengine na kuhakikisha kuwa taratibu na nyenzo za kazi za utawala zinatosheleza katika kutekeleza majukumu yake;
  • Kuwezesha habari zinazohusu Uongozi wa Dayosisi kuwafikia wote wanaohusika kwa wakati na kwa ukamilifu ili kudumisha maelewano baina yake na wenzake na pia baina ya Ofisi Kuu ya Dayosisi na Kamati na Halmashauri mbalimbali za Dayosisi pamoja na Vituo, Asasi, ofisi za Majimbo, Sharika na Mitaa;
  • Kuhakikisha mikutano katika ngazi zote na kila Idara inafanyika kulingana na taratibu zilizowekwa na kwa ufanisi;
  • Kuitisha Mkutano Mkuu, Halmashauri Kuu na Halmashauri ya Utendaji endapo Askofu au Msaidizi wa Askofu hawataweza kuitisha vikao hivyo kutokana na sababu maalum;
  • Kutembelea Sharika, Mitaa na Vituo vya Dayosisi mara kwa mara ili kukagua maendeleo na kupashana taarifa mbalimbali;
  • Kuratibu na kusimamia mipango na miradi ya maendeleo na ya Uchumi ya Dayosisi;
  • Kutunza maandishi, hati muhimu, mihuri ya Dayosisi (Seal) na kumbukumbu za Dayosisi;
  • Kwa kushirikiana na Askofu atatayarisha ajenda za Mikutano ya Halmashauri ya Utendaji, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu wa Dayosisi; Kutekeleza mapatano ya Mkutano Mkuu, Halmashauri Kuu na Halmashauri ya Utendaji;
  • Anaweza kuhudhuria vikao vya Bodi za Dayosisi, Kamati za Dayosisi na vya ngazi zote ndani ya Dayosisi;
  • Kutunza na kutangaza takwimu zote za Dayosisi kadri itakavyohitajika;
  • Kuwa mmojawapo wa wadhamini wa mali na rasilimali za Dayosisi; Atawakilisha Dayosisi katika vikao atakavyotakiwa kuhudhuria ndani na nje ya Dayosisi;
  • Kwa kushirikiana na Naibu Katibu Mkuu Mipango na Fedha, atasimamia mapato na matumizi ya fedha na mali zote za Dayosisi;
  • Kupokea na kutekeleza wajibu wowote mwingine kadri atakavyoagizwa na Askofu au Msaidizi wa Askofu;
  • Ataratibu utendaji wa watumishi wote wa DMP;

 

Sifa za Mwombaji

  • Awe Mkristo Mlutheri mwenye wito na umri usiopungua miaka arobaini (40);
  • Awe na Elimu yenye kiwango kisichopungua Shahada kwanza ya Chuo Kikuu kinachotambulika katika fani zifutazo: Sheria, Uchumi, Sayansi ya Jamii, Theolojia au mambo ya Utawala/Uongozi ikifuatiwa na Uzoefu kazini usiopungua miaka mitano (5) katika kazi ya Utawala;
  • Awe mwadilifu na mwaminifu;

 

Muda wa Mkataba

  • Katibu Mkuu atateuliwa kwa ushindani kwa mujibu wa Kanuni ya Utumishi na atakapoteuliwa na Halmashauri Kuu atakuwa madarakani katika kipindi cha miaka minne (4), ambacho kutokana na utendaji kazi kinaweza kuongezwa kipindi kingine cha miaka minne na cha mwisho, yaani vipindi viwili.
  • Pamoja na Masharti mengine yaliyowekwa katika Kanuni za Utumishi, Katibu Mkuu atakuwa hayuko madarakani ikiwa ataondoka au kuondolewa katika ajira ya Dayosisi;

 

No comments:

Post a Comment