Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP) ni moja ya dayosisi ishirini za
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Dayosisi hiyo
ilianzishwa na kusajiliwa mnamo 13 Desemba 1962 na wakati huo
ulijulikana kama Sinodi ya Uzaramo-Uluguru. Mnamo Desemba 1970 jina
lilibadilishwa kuwa KKKT Synod ya Mashariki na Pwani hadi Desemba 1986
wakati ikabadilishwa kuwa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani.
Shughuli za misioni katika maeneo ya pwani zilianza mnamo Agosti 1887
wakati mmisionari Johann Jacob Greiner kutoka misioni ya Berlin alifika
Dar es Salaam.
Dayosisi hiyo imepokea wito wake kutoka kwa Mungu mwenyewe, miongozi
mingine ni kanuni za KKKT, katiba ya dayosisi pamoja na katiba na sheria
za nchi. Kwa kutimiza katiba na sheria za nchi KKKT Dayosisi ya
Mashariki na Pwani imesajiliwa kisheria kama shirika la kidini nchini
Tanzania na kupewa cheti cha usajili No.10525 ya 25/8000.
Eneo la kazi yetui ni Mkoa wa Dar es Salaam, Mkoa wa Pwani na visiwa
vya Unguja, Pemba na Mafia. Jiografia hii imetuweka katika jiji kubwa la
Dar es Salaam ambayo ni kivutio kikubwa kwa watu kutoka sehemu mbali
mbali za Dunia.
Jiji ni kitovu cha kiuchumi cha nchi likiwa na nafasi nyingi kwa dayosisi na nchi yetu.
KKKT-DMP inashirikiana na inafanya kazi kwa karibu na Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na shirika zisizo za serikali za ndani ya nchi. Pia
inafanya kazi kwa kushirikiana au kwa uhusiano wa karibu na mashirika
ya kimataifa na ya nchi kwenye bara za Afrika, Asia, Ulaya na Amerika.
No comments:
Post a Comment