Wakulima Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, wamempongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kuelekeza ununuzi wa mazao yao kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.
Pongezi hizo walizitoa mwishoni mwa wiki wakati wa ulipwaji wa fedha zao baada ya kuuza choroko kwa njia ya stakabadhi ghalani katika Kata ya Iglanson.
” Kipekee nimshukuru Rais Magufuli kwa kuelekeza matumizi ya mfumo huu wa stakabadhi ghalani kwani umekuwa ni mkombozi kwa wakulima wetu.” alisema Mpogolo.
Alisema katika wilaya hiyo wakulima zaidi ya 500 wamenufaika na mfumo huo ambapo wameweza kupata zaidi ya sh.milioni 139 na kuokoa zaidi ya sh.milioni 54 ambazo wangenyonywa wakulima.
Mpogolo alisema changamoto kubwa iliyokuwepo ni walanguzi hao kujikita kwenye maeneo ya vijiji na kuupinga mfumo huo kwa kuwa ulikuwa ukiwanufaisha kwa miaka mingi.
lisema wachuuzi walikuwa wanatumia vipimo feki kwani utakuta katika kilo 50 zitazopimwa na mkulima utaona kilo tatu zilikuwa zikikatwa kiujanja na walanguzi hao. Huku wachuuzi wakinunua kilo moja kati ya sh.400 hadi 600 lakini kwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani waliweza kuuza kwa sh.1075 kwa kilo kwenye mnada wa tarehe 14 mwezi Mei 2020.
Mpogolo alitaja changamoto nyingine kuwa ni walanguzi hao kuwalaghai wakulima kuwa vyama vya ushirika vilikiwa havina uwezo wa kuwalipa fedha zao siku hiyo hiyo wakati sio agizo la mfumo.
Akimuongelea mkulima Joyce Nzela ambaye alitoa malalamiko kwa Rais Magufuli wakati alipo simama kwa muda na kuongea na wananchi wakati akiwa njiani kuelekea Dodoma akitokea Chato, ambaye alilalamikia mfumo wa ununuzi wa zao hilo alisema walipofuatilia hakuonekana katika orodha ya wakulima waliopeleka choroko kwenye AMCOS ya Kijiji cha Mayaha kama alivyodai. Hata hivyo kumbukumbu zilionyesha kwenye mkutano wa kutoa elimu ya mfumo uliofanyika Mei Mosi 2020 Kijiji cha Mtavila kuwa Joyce, alikuwa miongoni mwa wachuuzi walioupinga mfumo na kuwataka wakulima wasiukubali.
” Tulifuatilia tuligundua jina lake halikuwepo kwenye orodha ya wakulima ambao walipaswa kulipwa lakini wenzake, Zuhura na Amina walikuwepo kwenye orodha ya AMCOS ya Iglanson na malipo yao yalikuwepo.” alisema Mpogolo.
SOURCE MUUNGWANA BLOG